Jeremiah 31:18-20


18 a“Hakika nimeyasikia maombolezo ya Efraimu:
‘Ulinirudi kama ndama mkaidi,
nami nimekubali kutii.
Unirudishe, nami nitarudi,
kwa sababu wewe ndiwe Bwana, Mungu wangu.
19 bBaada ya kupotea, nilitubu;
baada ya kuelewa, nilijipiga kifua.
Niliaibika na kuona haya
kwa sababu niliibeba aibu ya ujana wangu.’
20 cJe, Efraimu si mwanangu mpendwa,
mtoto ninayependezwa naye?
Ingawa mara kwa mara ninanena dhidi yake,
bado ninamkumbuka.
Kwa hiyo moyo wangu unamwonea shauku,
nina huruma kubwa kwa ajili yake,”
asema Bwana.
Copyright information for SwhNEN